Rasilimali za Msingi Stadi za maisha

Rasilimali Za Msingi Stadi Za Maisha-PDF Download

  • Date:29 Jan 2020
  • Views:52
  • Downloads:0
  • Pages:14
  • Size:379.13 KB

Share Pdf : Rasilimali Za Msingi Stadi Za Maisha

Download and Preview : Rasilimali Za Msingi Stadi Za Maisha


Report CopyRight/DMCA Form For : Rasilimali Za Msingi Stadi Za Maisha


Description:

Transcription:

TESSA Teacher Education in Sub Saharan Africa inalenga. kuboresha utekelezaji darasani wa walimu wa msingi na walimu. wa sayansi wa sekondari barani Afrika kupitia matoleo ya. Rasilimali Huria za Elimu OERs ili kuunga mkono walimu. kuunda njia zinazowalenga wanafunzi na kuwashirikisha OER ya. TESSA huwapa walimu kitabu cha kurejea pamoja na vitabu vya. shule Zinatoa shughuli kwa walimu kujaribu madarasani pamoja na wanafunzi wao pamoja na. masomo ya utafiti inayoonyesha jinsi walimu wengine wamefunza mada hiyo na rasilimali. husishi za kuwaunga mkono walimu katika kukuza mipango ya masomo yao na ufahamu wa. OER ya TESSA imeandikwa kwa ushirikiano wa waandishi wafrika pamoja na wa kimataifa ili. kushughulikia mtalaa na muktadha Zinapatikana kwa matumizi ya mtandaoni na chapa. http www tessafrica net OER Msingi zinapatikana katika matoleona lugha kadhaa. Kiingereza Kifaransa Kiarabu na Kiswahili Mara ya kwanza OER ilitolewa kwa Kiingereza. na kupatikana Afrika nzima OER hizi zimebadilishwa na washirika wa TESSA ili kufaa Ghana. Nijeria Zambia Rwanda Uganda Kenya Tanzania na Afrika Kusini na kutafsiriwa na. washirika nchini Sudani Kiarabu togo Kifaransa na Tanzania Kiswahili OER ya Sayansi ya. Sekondari zinapatikana kwa Kiingereza na zimebadilishwa ili kufaa Zambia Kenya Uganda na. Tanzania Tunakaribisha maoni kutoka kwa wale wanaosoma na kutumia rasilimali hizi Leseni. ya uundaji wa ubunifu huwawezesha watumiaji kuchukua na kujanibisha OER zaidi ili kutimiza. mahitaji na muktadha wa kindani, TESSA inaongozwa na Open University Uingereza na inafadhiliwa kwa sasa na ruzuku za. ufadhili kutoka kwa Wakfu wa Allan and Nesta Ferguson Wakfu wa William and Flora Hewlett. na Open University Alumni Orodha kamili ya wafadhili inapatikana kwenye tovuti ya TESSA. http www tessafrica net, Pamoja na rasilimali kuu za mafundisho za kuunga mkono mafunzo katika masomo maalum ni. chaguo za rasilimali za ziada ikiwa ni pamoja na sauti rasilimali kuu ambazo zinafafanua. utendakazi vitabu na zana maalum,TESSA Programme,The Open University. Walton Hall,Milton Keynes MK7 6AA,United Kingdom,tessa open ac uk. Copyright 2017 The Open University, Except for third party materials and otherwise stated this content is made available under a Creative Commons.
Attribution Share Alike 4 0 licence http creativecommons org licenses by sa 4 0 Every effort has been made to. contact copyright holders We will be pleased to include any necessary acknowledgement at the first opportunity. TESSA SwPA LS M3 S4 August 2017, This work is licensed under a Creative Commons Attribution Share Alike 4 0 License. Sehemu ya 4 Kutalii mazingira 4,Somo la 1 4,Somo la 2 6. Somo la 3 7, Nyenzo rejea ya 1 Matatizo ya upatikanaji wa maji 9. Nyenzo rejea ya 2 Shajara ya matumizi ya maji 9,Nyenzo rejea 3 Hadithi ya mkulima mchoyo 9. Nyenzo rejea 4 Maswali kuhusu utumizi wa ardhi 11,Nyenzo rejea 5 Sebastian Chuwa 11.
Creative Commons Attribution Share Alike www tessafrica net. TESSA SWAHILI Stadi za maisha Moduli 3 Sehemu ya 4. Page 3 of 14,Sehemu ya 4 Kutalii mazingira, Swali Lengwa muhimu Utapataje takwimu ili kuendeleza ujifunzaji wa wanafunzi kuhusu. Maneno muhimu mazingira kukusanya data tathmini shajara hadithi za maisha halisi. Matokeo ya ujifunzaji,Mwishoni mwa sehemu hii utakuwa umeweza. Kutumia hadithi halisi umekusanya data na umeandika shajara ili kuendeleza. welewa wa masuala ya mazingira, Kupanga kutekeleza na kutafakari utendaji kuhusu masuala ya mazingira. Kutathmini ujifunzaji wa darasa na mafanikio ya mradi. Utangulizi, Suala muhimu duniani ni athari za watu kuhusu mazingira Tukit umia vibaya rasilimali na. kuchafua mazingira kutakuwa na athari hasi kwa wanyama na mimea na hivyo tutaifanya. dunia iwe hatari kwa vizazi vijavyo, Ukiwa mwalimu na raia mwema unahitaji kuelewa masuala ya mazingira na kuchukua hatua.
kama mfano kwa wanafunzi wako na kuwasaidia kuelewa masuala haya Unaweza kufanya. hivyo kwa kuwapa shughuli ambazo zinahusisha ukusanyaji wa taarifa kuhusu mazingira. katika sehemu zao au katika sehemu pana zaidi na kutumia taarifa hizo kufikiria kuhusu. matokeo ya matendo mbalimbali, Kujifunza baadhi ya dhana tata kuhusu mazingira kunakuhitaji wewe ukiwa mwalimu kuziweka. dhana hizo katika vipengele vidogovidogo na kujenga picha kamili Wanafunzi wanaelewa zaidi. kama watafikiria juu ya mawazo wanayoyajua na kutumia mazingira yanayowazunguka. kuwaonesha jinsi mawazo hayo yanavyohusiana na hali yao. Kuna njia nyingi za kufanya hivi Sehemu hii inatilia mkazo ukusanyaji wa taarifa kutokana na. ujuzi wa wanafunzi kutalii dhana na majukumu na haki zao. Creative Commons Attribution Share Alike www tessafrica net. TESSA SWAHILI Stadi za maisha Moduli 3 Sehemu ya 4. Page 4 of 14, Uchunguzi kifani ya 1 Utafiti kuhusu matumizi ya maji katika. Mwalimu Namhlane wa Nigeria alikuwa anaanza mada na wanafunzi wake wa darasa la pili. kuhusu mazingira akizingatia umuhimu wa maji katika maisha ya kila mmoja wetu. Ili kuwahamasisha wanafunzi wake kuhusu mada hii alianzisha mradi wa darasa Kwanza. aliwataka waunde vikundi vya watu sita hadi wanane wanaoishi katika sehemu moja ya jamii. na kuwaeleza kuwa kuna wageni watatu wanakuja shuleni siku inayofuata mmoja akitoka. kila sehemu ya jamii ili kuzungumzia wanavyopata na kutumia maji Aliwataka wanafunzi. wake kufikiria na kuandika maswali watakayouliza Makundi haya ya sehemu ya jamii. yalishirikiana maswali yao ili kuhakikisha kuwa kila kikundi cha sehemu kingeweza kuona. kama limefikiria vipengele vyote, Kesho yake kila mgeni alizungumza na wanafunzi wanaotoka katika sehemu yake ndani ya. darasa au nje chini ya mwembe Vikundi viliuliza maswali kwa njia tofauti katika kikundi. kimoja wanafunzi tofauti waliuliza swali moja kila mmoja na katika kikundi kingine mvulana. na msichana waliuliza maswali yote na waliobaki waliandika majibu. Baada ya wageni kuondoka wanafunzi walitakiwa kuorodhesha mambo matatu muhimu. waliozingatia na kuwaelezea darasa zima Mwalimu Namhlane alikitaka kila kikundi kwa. zamu kuelezea walichogundua lakini bila kurudia jibu lililokwisha andikwa ubaoni. Baada ya hapo walijadili matatizo yaliyokuwepo kuhusu maji na kufikiria jinsi ya kutatua. Tazama Nyenzo rejea 1 Matatizo ya kupata maji, Shughuli ya 1 Uwekaji wa kumbukumbu katika shajara ya maji. Watake wanafunzi wako kuweka kumbukumbu katika shajara kwa muda wa wiki moja. Wataandika labda karatasi kubwa ya ukutani kiasi cha maji wayatumiayo na kwa matumizi. yapi Tazama Nyenzo rejea 2 Shajara ya matumizi ya maji kwa ajili ya kiolezo cha. Baada ya wiki moja watake kufanya kazi katika vikundi na kuorodhesha katika yao matumizi. yote ya maji na yaorodheshe kwa kuzingatia ni shughuli zipi zinatumia maji kwa wingi zaidi na. zipi zinatumia maji kidogo Bandika orodha hiyo ukutani na waruhusu kusoma kazi za wenzao. kabla ya kuwa na majadiliano ya pamoja ya mwisho wakijadili masuala yahusuyo maji katika. sehemu zao, Itakuwa vyema kufikiria maswali kama Maji yote yanapatikana kutoka wapi Je kila.
mmoja anapata maji Je maji yetu ni safi na salama Huduma zetu za maji zinaweza. kuboreshwaje Tunaweza kusaidiaje, Unaweza kuhusisha shughuli hii na kazi za tarakimu kwa kuangalia data kiasi cha maji. kilichotumika sayansi kwa nini maji ni muhimu katika maisha yetu na masomo ya jamii. matatizo ya kupata maji katika baadhi ya sehemu za Afrika. Creative Commons Attribution Share Alike www tessafrica net. TESSA SWAHILI Stadi za maisha Moduli 3 Sehemu ya 4. Page 5 of 14, Kuchora ni njia nzuri ya kutambua mawazo ya wanafunzi kuhusu mada yoyote Inawawezesha. kuonesha mawazo yao bila kulazimika kuzungumza kwa sauti au kuweza kuandika Ni njia. nzuri kwa vijana wadogo na huwapatia njia ya kuzungumza maoni yao Si lazima michoro iwe. ya kiwango cha juu bali isimulie hadithi au ioneshe wazo Kwa kutumia hadithi ni njia nyingine. ya kuwaham asisha wanafunzi kufikiri kwa kina kuhusu tatizo Inaondoa hali ya kumlenga mtu. mmoja na badala yake inawawezesha wanafunzi kuzungumza kwa uwazi zaidi Hadithi. zinaweza pia kutoa taswira kubwa zaidi kwa wanafunzi na kuwahamasisha Uchunguzi kifani. 2 na Shughuli ya 2 vinaonesha jinsi unavyoweza kutumia mbinu zote mbili katika darasa lako. Uchunguzi kifani ya 2 Hadithi na masuala ya mazingira. Mwalimu Ngede aliwasomea wanafunzi wake Nyenzo rejea 3 Hadithi ya mkulima mwenye. ubinafsi ili kuhamasisha mawazo yao kuhusu ulimwengu na rasilimali zake. Baada ya hapo aliwapa karatasi na kuwataka wachore picha ya kwa nini mkulima alikuwa. Aliwaelezea wazo hili kwa makini na kuwahamasisha wasinakili bali kufikiria juu ya mawazo. yao Baada ya wanafunzi kumaliza kuchora walibandika picha zao ukutani Mwalimu Ngede. aliwataka baadhi ya wanafunzi kueleza picha zao zilihusu nini na alijaribu kukisia zingine. zilihusu nini Wanafunzi walifurahia sana zoezi hili. Baadaye aliongoza majadiliano kuhusu umuhimu wa kila mmoja kutunza ardhi. Waliorodhesha pamoja ubaoni jinsi watu katika jamii yao walivyotumia ardhi na jinsi. walivyoitunza, Baadaye aliwauliza maswali ambayo waliyajadili katika vikundi Kwa mfano. Watu walitumiaje ardhi Waliitunza Ni kwa njia ipi mkulima angeitunza ardhi hii Nani. alifanya kazi Je ardhi ilikuwa na rutuba Kama ndivyo kwa nini Kama sivyo kwa nini. Wanaweza kuboresha jinsi wanavyoitunza ardhi, Mengi yanaweza kupatikana katika Nyenzo rejea 4 Maswali kuhusu matumizi ya ardhi. Kama darasa walifikiria maswali haya na kutoa mawazo yao. Mwishoni mwa siku Mwalimu Ngede aliwataka wanafunzi wakati wakiwa wanaelekea. majumbani kwao waangalie njia mbalimbali za matumizi ya ardhi na kesho yake waje na. mawazo yoyote ambayo yanaweza kuongezwa katika orodha yao. Creative Commons Attribution Share Alike www tessafrica net. TESSA SWAHILI Stadi za maisha Moduli 3 Sehemu ya 4. Page 6 of 14,Shughuli ya 2 Viongozi na mazingira, Shughuli hii inazingatia kwa upana zaidi umuhimu wa kutunza mazingira.
Nyenzo rejea 5 Sebastian Chuwa anasimulia habari za Mtanzania mmoja aliyehamasisha. jamii kujiunga pamoja kutatua matatizo ya mazingira Soma habari hii kabla hujaanza. kutayarisha somo, Wasimulie habari hii wanafunzi wako Andika ukutani tahajia za maneno kwa mfano. hifadhi ya mazingira, Baada ya kusoma hadithi jadili maneno hayo na maana zake. Watake wanafunzi wako wakiwa wawili wawili wajifikirie kama Sebastian Chuwa Ni masuala. yapi ya mazingira ambayo wangependa kuyafanyia kazi Wangefanyaje Zunguka darasani. na waulize wanafunzi walio katika vikundi vya watu wawiliwawili wenye mawazo mazuri. kuyaeleza kwa wenzao darasani, Watake wachunguze mazingira yao wakati wa kurejea nyumbani na waone kama kuna. masuala mengine ambayo hawakuyaona kabla na wayazungumzie kesho yake Orodhesha. masuala matano wanayoyapendelea, Ukiwa mwalimu unahitaji kuwasaidia wanafunzi wako kuelewa majukumu yao kuhusu. mazingira katika hali ambayo inawahamasisha na kuendeleza mtazamo wa kuyatunza Katika. Shughuli Muhimu bango linatumika kama kichocheo na katika Uchunguzi kifani 3 mradi. mdogo umeelezwa ambao unaonesha jinsi vikundi tofauti vinavyoweza kushirikiana ili kuleta. mabadiliko, Wakati wanafunzi wanaendelea kushughulikia mradi huo kazi yako ni kuwa umejitayarisha.
kutarajia baadhi ya mahitaji yao na kuwapa nyenzo ili kusaidia kujifunza kwao Kama una. darasa kubwa unahitaji kufikiria jinsi utakavyowashirikisha wanafunzi wako wote na labda. kugawanya kazi katika makundi Kwa wanafunzi wa umri mdogo utatakiwa kufanya shughuli. za kiwango kidogo na washirikishe baadhi ya wanajamii wakusaidie zaidi. Creative Commons Attribution Share Alike www tessafrica net. TESSA SWAHILI Stadi za maisha Moduli 3 Sehemu ya 4. Page 7 of 14, Uchunguzi kifani ya 3 Upangaji na utekelezaji wa kampeni. Darasa la shule ya Ngombe Iringa liliamua kampeni ya usafi Mwalimu wao aitwaye mama. Mboya amekuwa akiufanyia kazi mtaala mpana wenye kichwa cha habari kulinda ardhi yetu. Baada ya kuzungukia shule asubuhi nzima na maeneo yanayoizunguka Mwalimu Mboya na. darasa lake walijadili waliyoyaona Waliorodhesha mambo yote waliyoyapenda katika sehemu. hizo na sehemu au mambo waliyotaka kubadili au kuboresha. Waliamua kufanyia kazi sehemu ndogo mbili kwa kuzisafisha uwanja wa shule wa michezo. na kijito kilicho karibu na shule, Darasa liligawanywa katika makundi mawili yakiwa na timu mbili zikifanya kazi katika kila. sehemu Timu zilijadili wanachoweza kufanya halafu zilishirikiana mawazo na timu nyingine. Walikubaliana nani atafanya kazi gani na kila timu ilitekeleza mipango yake kwa muda wa. juma zima wakati wa saa za shule, Darasa lilifanya usafi kwa muda wa wiki nzima Baadaye walifanya maonesho katika ukumbi. wa shule ambayo yalionesha, Wingi na aina za takataka zilizokusanywa wakati wa kufanya usafi Mipango ya kuendeleza. hali ya usafi na kutokuwa na takataka katika siku zijazo Jinsi ya kushughulikia takataka ikiwa. ni pamoja na kuzitumia tena kwa shughuli nyingine baada ya kuzipitisha katika mchakato. mwingine au kuzifukia au kuzichoma, Maonesho yalifanikiwa na wanafunzi wa madarasa mengine walifurahia kazi iliyofanywa na.
kusaidia kuweka shule safi zaidi, Shughuli muhimu Kuchukua hatua kuhusu masuala ya mazingira. Shughuli hii ni mwendelezo wa uhamasishwaji wa wanafunzi wa kushughulikia masuala ya. takataka na inachukua mbinu ya hatua kwa hatua ya kujifunza kwa vitendo. Hatua ya 1 Watake wanafunzi labda katika vikundi vya wawiliwawili kutambua masuala ya. takataka shuleni na karibu na shule Chagua kipengele labda kile kilichotajwa mara nyingi. Hatua ya 2 Shirikiana na darasa kutayarisha mpango wa utekelezaji Ili kufanya shughuli. hii kitake kila kikundi kupendekeza njia za kutatua matatizo Hakikisha kuwa mpango wa. utekezaji uliokubalika ni halisi na unaweza kutekelezwa na darasa Wape wanafunzi katika. vikundi kazi za kufanya Uandike mpango wa utekelezaji katika bango likionesha mwisho wa. utekelezaji bango hilo linaweza kuwekwa katika ukuta wa darasa. Hatua ya 3 Chukua hatua hii inaweza kuwa kazi ya siku au miezi mingi lakini hakikisha. kuwa kila kikundi kinaweka kumbukumbu za kila wanachokifanya lini na kwa utaratibu upi. Hatua ya 4 Wakiwa wanakamilisha kila sehemu ya mpango huo wa utekelezaji watake. warekodi maendeleo yao katika bango, Hatua ya 5 Wakati wakimalizia tafakari mafanikio ya mpango pamoja na darasa. Wamejifunza nini Kulikuwa na matatizo gani Watafanya nini kuendeleza wazo hili Je. sehemu imeendelea kuwa safi, Creative Commons Attribution Share Alike www tessafrica net. TESSA SWAHILI Stadi za maisha Moduli 3 Sehemu ya 4. Page 8 of 14,Nyenzo rejea ya 1 Matatizo ya upatikanaji wa maji. Mfano wa kazi ya wanafunzi Nyenzo rejea ya Mwalimu ya kutumia katika. kupanga au kurekebisha pamoja na wanafunzi,Umbali wa kusafiri kutembea ili kupata maji.
Kuwaacha watoto wadogo nyumbani na kwenda kutafuta maji. Wanafunzi kutokwenda shule kwa ajili ya kwenda kuchota maji. Je maji ni safi na salama, Ujazo wa vyombo vya kuchotea maji na uzito wa kubeba kwa masafa marefu. Muda unaotumika kutafuta maji unawazuia watu kufanya mambo mengine. Maji yanayochotwa yanaweza kuwa yamechanganyika na uchafu na kutumiwa. na wanyama, Hatari ya maambukizi ya magonjwa yanayosababishwa na utumiaji wa maji. Ukame unaweza kukwamisha upatikanaji wa maji safi, Ukosefu wa miundombinu k v mabomba na vyombo vya kuhifadhia maji. yatokanayo na mvua n k,Ukosefu wa mifumo ya kusafisha maji. Ukosefu wa elimu kuhusu njia za kutumia na kutunza rasilimali asilia za. maji vyanzo vya maji,Hakuna upatikanaji endelevu wa maji.
Nyenzo rejea ya 2 Shajara ya matumizi ya maji,Matumizi ya wanafunzi. Kila wakati unapotumia maji kwa kunywa au kupikia n k weka alama ya tiki katika kisanduku. kinachostahili,Kunywa Kupikia Kufulia Kusafishia nyumba Mengine. Creative Commons Attribution Share Alike www tessafrica net. TESSA SWAHILI Stadi za maisha Moduli 3 Sehemu ya 4. Page 9 of 14,Nyenzo rejea 3 Hadithi ya mkulima mchoyo. Nyenzo rejea za mwalimu kwa ajili ya kupanga na kutumia na wanafunzi. Kulikuwa na mkulima mmoja kijana Alikuwa na mke na watoto wawili na waliishi katika kijiji. kidogo Mkulima alirithi shamba lake kutoka kwa babu yake aliyekuwa mchapakazi na ambaye. alimpenda sana Ingawa alikuwa na huzuni kwa kifo cha babu yake mkulima aliridhika kwa. kuwa mmiliki pekee wa ardhi yote, Alikuwa ni kijana mchapakazi na aliweza kulitunza shamba vizuri kama si vizuri zaidi kuliko. babu yake Alijifunza mengi kutoka kwa babu yake lakini pia alijifunza vema shuleni na alisoma. mambo mengi kuhusu njia mbalimbali za kuhifadhi maji na kutunza ardhi jambo ambalo. liliongeza mazao yake Hata hivyo hakuwa kama babu yake kwa kuwa hakuwagawia wakulima. na wazalishaji wengine pale kijijini mawazo au mazao yake ya ziada. Wanakijiji walishangaa walipokwenda kumwomba mbegu au ushauri kwa kuambiwa kwamba. watoke katika ardhi yake Mke wake hakupenda tabia hii lakini aliheshimu mawazo ya. mumewe Wanakijiji walitazama alichofanya na baadhi wakajaribu kuiga mambo aliyoyafanya. bila kupata mafanikio makubwa Wengine walicheka au kunung unika kwa aliyoyafanya. Wakati mmoja wa msimu wa kiangazi mazao hayakustawi vizuri katika kijiji kile Kulikuwa na. maji kidogo kwa sababu kijito kilikauka hivyo kulikuwa na mwendo mrefu wa kilometa sita. kuelekea kwenye chanzo kingine cha maji Maana yake ni kwamba maji yaliyoletwa nyumbani. yalitumika kwa kunywa tu, Hata hivyo mkulima mchoyo alikuwa na maji na chakula kingi lakini hakuwasaidia wanakijiji.
ambao walikuja kuomba msaada Mkewe alimwomba awasaidie lakini hakubadili msimamo. wake Alitengeneza mifereji na kingo ili kukusanya maji ya mvua na aliyahifadhi katika mapipa. makubwa ambayo alikuwa nayo Kwa hiyo ukame ulipotokea aliweza kumwagilia mimea yake. ambayo ilikua vizuri kama kawaida, Jinsi kulivyoendelea kuwa na joto na kiangazi kikali mazao ya watu yalianza kufa na watu. wengi wakapatwa na njaa Mke alijaribu kumshawishi mumewe awasaidie wanakijiji Watoto. walijaribu kumshawishi baba yao lakini hakuwasikiliza Alisema alifanya kazi kwa bidii hivyo. mazao ni mali yake na wengine walikuwa wavivu au hawakuangalia yatakayotokea mbele. Hata hivyo siku moja mtu aliyekonda sana na mwenye nguo zilizoraruka alifika shambani. kuomba msaada wa chakula kwa ajili ya mke wake ambaye alikuwa mgonjwa Mkulima. alimfukuza kwa ukali lakini mke wake alimzuia na kusema Humtambui mpwa wako Mkulima. alipatwa na mshtuko kwa jinsi mpwa wake alivyoonekana amekonda na amezeeka Mpwa. alielezea jinsi alivyojaribu kutunza maji lakini alishindwa na jinsi mazao yake yalivyokufa. Mkulima akamweleza anachotakiwa kufanya wakati mwingine Lakini mke wake akasema. amedhoofika mno kiasi cha kushindwa kufanya hayo vinginevyo umpe chakula yeye na mke. wake Mkulima alitulia na akampa mpwa wake chakula Mpwa alirudi wiki iliyofuata akasema. mkewe amepata nafuu na kuomba chakula zaidi Mkulima alitaka kukataa lakini mkewe. akamwambia kwamba walikuwa na njaa sana kwa hiyo haikutosha kuwapa fungu moja tu la. chakula Mkulima aliwapa chakula na katika kipindi cha siku chache zilizofuata taratibu. alibadilika mawazo yake baada ya kutafakari kuhusu uchoyo na utovu wa busara kuhusiana na. kumbukumbu ya babu yake na shida ya majirani zake Kwa hiyo aliwaita wanakijiji shambani. kwake akawagawia chakula na kuahidi kuwasaidia kujiandaa vizuri kwa ajili ya msimu ujao wa. Creative Commons Attribution Share Alike www tessafrica net. TESSA SWAHILI Stadi za maisha Moduli 3 Sehemu ya 4. Page 10 of 14,Nyenzo rejea 4 Maswali kuhusu utumizi wa ardhi. 1 Ardhi inaweza kutumika kwa njia ngapi tofauti Ziorodheshe. 2 Kwa nini ni muhimu kutunza ardhi, 3 Kwa nini watu wengine ni wachoyo zaidi kuliko wengine Kwa nini ni lazima. tugawane ardhi yetu, 4 Tunawezaje kuwahamasisha watu kuhusu tabia ya kugawana Je ni lazima. tugawane kila kitu,5 Je tunatunza ardhi yetu vizuri.
6 Ni nani mwingine tunagawana naye ardhi yetu, 7 Ni kwa jinsi gani tunaweza kutunza ardhi yetu vizuri. 8 Sisi tukiwa wanadarasa tunaweza kufanya nini ili tutunze ardhi ya shule. Nyenzo rejea 5 Sebastian Chuwa, Nyenzo rejea za mwalimu kwa ajili ya kupanga na kutumia na wanafunzi. Sebastian Chuwa ni mtu mwenye ndoto kwa nchi yake watu wake na vizazi vijavyo ambao. watarithi urithi wao Kwa miaka 30 amekuwa mstari wa mbele kusomea matatizo ya mazingira. katika ardhi yake ya nyumbani Tanzania Afrika ya Mashariki na majawabu aliyoyapata. yanatoa matokeo yanayonufaisha si ardhi peke yake bali watu wote wanaotegemea ardhi kwa. maisha na maendeleo yao Mbinu zake ambazo zimejikita katika malengo ya msingi mawili ya. uhamasishaji kwa vitendo katika jamii kuratibu zoezi la watu kueleza matatizo yao katika. ngazi ya mtaa na elimu kwa vijana ili kuhamasisha ufundishaji wa uhifadhi wa ardhi. mashuleni kuanzia ngazi ya shule za msingi, Creative Commons Attribution Share Alike www tessafrica net. TESSA SWAHILI Stadi za maisha Moduli 3 Sehemu ya 4. Page 11 of 14, Ametoa msukumo kwa makundi makubwa ya vijana wa kujitolea wa kijumuia kukaa pamoja na. kutatua sio tu matatizo yao ya kimazingira bali pia matatizo yao ya kupunguza umasikini. kuwawezesha wanawake na maendeleo ya vijana katika eneo la Mkoa wa Kilimanjaro. kaskazini mwa Tanzania Juhudi zake kwa niaba ya shirika la African blackwood zimeunda. mpango wa kwanza wa kiwango cha juu wa kupanda upya wa spishi za mimea Kwa sababu. ya uanzishwaji wa bustani nyingi za miche ya miti za kijumuia na miradi kadhaa ya ushirika. inayokusudia kuboresha kupanda upya kwa miti kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita mwaka. 2004 ABCP na makundi ya vijana walioshiriki katika kazi ya Sebastian walisherehekea. upandaji miti milioni moja, Aina ya kazi yake ambayo inapanuka kila wakati imempa yeye na jumuia yake hadhi ya kuwa.
viongozi katika uwanja wa hifadhi ya Tanzania, Historia ya Mradi wa Hifadhi wa African Blackwood African Blackwood Conservation Project. Mwaka 1996 James Harris mtaalamu wa kutengeneza mapambo kutoka Texas USA na. Sebastian Chuwa walifadhili Mradi wa Hifadhi wa African Blackwood ABCP ili kuanzisha. mpango wa elimu na upandaji upya wa miti hasa kwa ajili ya spishi ya mmea uitwao mpingo. Dalbergia melanoxylon katika eneo lake la nyumbani lililoko mashariki mwa Afrika Mti wa. mpingo unatumiwa sana na wachongaji wa Kiafrika na watengenezaji wa vifaa wa Ulaya kwa. ajili ya kutengeneza zumari filimbi na vifaa vingi vingine vya muziki Kwa sababu ya kuvunwa. kupita kiasi na kukosekana kwa juhudi zozote zinazoelekezwa kwenye kupanda upya kwa. spishi hii kuendelea kuwepo kwake kuko hatarini, Mwaka1995 James Harris ambaye anatumia mpingo katika sanaa zake za mikono aliona. filamu ya The Tree of Music huko Marekani na alidhamiria kufanya jambo kuhusiana na. uhifadhi wa spishi hii Aliwasiliana na Sebastian kwa barua pepe na alipendekeza washirikiane. angezindua mpango wa kuchangia mfuko miongoni mwa wazalishaji wa bidhaa za miti. wanamuziki wahifadhi misitu wa nchi za magharibi na kisha kutuma fedha zitakazopatikana. kwa Sebastian ili aanzishe bustani ya miti nchini Tanzania Mradi uliidhinishwa na Bwana. Chuwa kwa shauku kubwa Tangu wakati wa mawasiliano hayo ya awali ABCP imekuwa ndiyo. nguvu inayoongoza uhifadhi wa mpingo kaskazini mwa Tanzania inayofadhili bustani za. mimea kwa ajili ya uzalishaji mkubwa wa miche ya mpingo na inayohamasisha kuhusu. umuhimu wa spishi ya mpingo kimataifa,Hifadhi ya Ngorongoro. Kifaru mweusi huzuia magari barabarani katika Hifadhi ya Ngorongoro. Creative Commons Attribution Share Alike www tessafrica net. TESSA SWAHILI Stadi za maisha Moduli 3 Sehemu ya 4. Page 12 of 14, Wakati wa utoto wake nyumbani kwa Sebastian Chuwa kulikuwa kwenye mteremko wa kusini. mwa Mlima Kilimanjaro katika kimo cha 4900 Alijifunza kupenda mambo ya asili tangu utotoni. kutoka kwa baba na mshauri wake Michael Iwaku Chuwa ambaye alikuwa mtaalamu wa. mitishamba Kwa pamoja walianzisha jitihada ya kusafiri na kufanya utafiti katika misitu ili. kukusanya mimea ya madawa ambayo baba yake aliyatumia kwa kazi yake Kutokana na. safari hizi katika kipindi cha miaka mingi alijifunza majina ya mimea na miti miongoni mwa. mimea yote iliyosheheni katika eneo la Kilimanjaro Upendo wake kwa dunia asilia unaendelea. mpaka leo na ndio siri inayoongoza kazi yake, Baada ya kumaliza elimu ya sekondari alisoma katika Chuo cha Usimamizi wa Maliasili cha.
Mweka na baada ya kuhitimu aliajiriwa kama mhifadhi katika Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro. Katika kipindi cha miaka 17 cha ajira yake hapo alijisomea na kuandika katalogi ya mimea ya. sehemu ile aligundua spishi mpya nne ambazo kwa heshima yake mbili kati ya hizo zimeitwa. jina lake na amekusanya hodhimadawa ya mitishamba yenye aina 30 000 za mimea katika. kituo cha wageni kwa ajili ya matumizi ya wageni na watumishi Kwa sababu ya welewa wake. mpana kuhusu mimea mingi ya eneo hilo anafanya kazi na Mary Leakey katika eneo la jirani la. Oldavai Gorge kuitambua mimea kwenye eneo la ugunduzi wa mtu wa mwanzo la Leakey Vile. vile katika Hifadhi ya Ngorongoro alianzisha mpango wa kuhifadhi vifaru weusi walio hatarini. kutoweka mpango ambao ulipata mafanikio Mpango huu ulinakiliwa katika sehemu nyingine. Mbuga ya Ngorongoro ni eneo ambalo linasimamiwa kwa ushirika ambako jamii za Wamasai. bado zinaishi na mifugo yao Wakati wa kipindi chake cha ajira katika Mbuga Sebastian. alifanya kazi kwa karibu na Wamasai akijifunza madawa yao na kuanzisha bustani za miti kwa. ajili ya matumizi yao Vile vile alianzisha mpango wa kwanza wa elimu ya hifadhi ya misitu kwa. vijana nchini Tanzania hasa kwa ajili ya watoto wa Kimasai uliohusu shughuli za kivitendo. kama vile uanzishaji wa bustani za miche ya miti na miradi ya upandaji wa miti Klabu hii. ilifanikiwa sana hata ikiwa mfano kwa harakati za upandaji miti za nchi nzima iliitwa Klabu ya. Malihai ya Tanzania iliyoanzishwa mwaka 1985 ikiwa na ofisi katika Makao Makuu ya Mbuga. ya Ngorongoro iliyoko Arusha hivi sasa inafanya kazi nchi nzima na ina klabu zipatazo 1 000. Ofisi na Tuzo, Mwaka 1999 Sebastian alitunukiwa wadhifa wa kuwa mwenyekiti wa Mfuko wa Dhamana ya. Usimamizi wa Hifadhi ya Mazingira Kilimanjaro na Mamlaka ya Serikali ya Mkoa wa. Kilimanjaro Tanzania Ofisi hii moja kwa moja inamfanya awe mjumbe wa Kamati ya Hifadhi. ya Mazingira ya Mkoa Kutokana na wadhifa huu michango yake muhimu katika hifadhi ya. mazingira itasambaa, Imetoholewa kutoka African Blackwood Conservation Project Website. Kurudi Stadi za maisha ukurasa, Creative Commons Attribution Share Alike www tessafrica net. TESSA SWAHILI Stadi za maisha Moduli 3 Sehemu ya 4.

Related Books